

Bagamoyo, Oktoba 10, 2025 — Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa yeye ni mzima na afadhali afya yake ipo nzuri.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati alipohudhuria mkutano wa kampeni za urais za Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, uliofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani.
Rais Kikwete, ambaye ametoa nafasi ya urais tangu mwaka 2015, aliwaambia wananchi waliofika kwenye mkutano huo kuwa yupo imara na ameendelea kushirikiana katika shughuli za kijamii na za kisiasa, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano wa kitaifa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!