Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Askofu Dallu Atangaza Kutoweka kwa Padri Camillus Nikata, Waomba Msaada wa Polisi – Video

  • 9
Scroll Down To Discover

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu, ametangaza kutoweka kwa Padri Camillus Nikata, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo, Askofu Dallu amesema kuwa Padri Nikata haonekani wala hapatikani kwa simu.

Askofu Dallu amesema padri alikuwa ametokea Dodoma kwenye mafundisho ya moyo ya mapadri wanaofundisha katika vyuo vikuu vya TEC, akiwa na mhadhiri mwenzake wa Jimbo.

Inaelezwa kuwa alipanga kusafiri kwenda Mwanza Oktoba 8, 2025 kwa basi la Super Feo, na tayari alikuwa amenunua tiketi kwa njia ya mtandao.

Taarifa inazidi kueleza kuwa, walipoanza kuangalia Jumatano mchana, waligundua kuwa hakusafiri kwani mzigo wake ulikuwa bado umebaki katika chumba chake kilichofungwa, na ufunguo haukurudishwa kwa mtumishi wa nyumba ya mapadri.

Jitihada za kumtafuta kwa simu na kuulizia kwa watu waliokuwa naye hazikuzaa matunda, na alikosekana pia Mwanza, mahali alipokuwa amepanga kufika.

Ofisi ya mabasi ya Super Feo ilithibitisha kuwa hakusafiri kwa basi hilo.

Baada ya kushindikana kwa jitihada za kumtafuta Padri Nikata, Askofu Dallu amesema kuwa tayari wameshatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili msaada zaidi upatikane na kumtafuta padri huyo.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Dkt. Samia Ahimiza Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mugumu Serengeti Kuendeleza Utalii – Video
Next Post Furaha kwa wakaazi wa Gaza wakati Israel ikisitisha vita, katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook