
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia msanii Mac Voice kuonekana akipiga Show za Chaka Tu Chaka.
Anasema sio jambo baya msanii kufanya hizo Shows maana atapata wapi hela bila kujituma Mikoani??
Kinachowafanya watu walalamike ni kwa sababu Standard aliyoi-set Rayvanny ndio maana wengi wanaona sio level zake.
Anasema Sio Mac Voice tu bali lebo nyingi sana hapa nchini Wasanii wao wanapitia katika hali mbaya sana ya Kiuchumi na pia hawana amani ya Kikazi.
Yote ni kwa sababu lebo hazikuzianzishwa kusaidia vijana na kufanya biashara bali zilianzishwa kushindana na WCB au Diamond.
Kadri siku zinavyoenda maji na mafuta yameanza kujitenga maana wasanii hawawekezi kwenye lebo zao, wengi wao wamefungua lebo kwa sababu ya sifa tu bila kujua wanaua vipaji vya vijana wengi.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!