Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Biteko: Tuzo Za Malkia Wa Nguvu Ni Chachu Ya Maendeleo Kwa Wanawake Na Jamii

  • 7
Scroll Down To Discover

Jukwaa la Malkia wa Nguvu la Clouds Media lilioanzishwa mwaka 2016 limeendelea kutimiza lengo lake la kuhamasisha na kuunga mkono wanawake katika nyanja za ujasiriamali, maendeleo ya kiuchumi na masuala mengine mbalimbambali ya kijamii kwa kipindi cha miaka tisa sasa.

Akizungumza Aprili 4, 2025 jijini Dar es salaam wakati aliposhiriki katika sherehe za Tuzo za Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema jukwaa hilo pia hutambua, huthamini na husherehekea jitihada na michango ya wanawake waliothubutu na kufanikisha maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii, uchumi na uongozi.

“ Tangu kuanzishwa kwake, hadi sasa, jukwaa hili limekuwa ni chachu kubwa ya maendeleo kwa wanawake na jami kwa ujumla. Naomba niwapongeze, Clouds Media Group kwa kazi hii nzuri. ” Amesema Dkt. Biteko

Amesisitiza “Kuanzisha na kuendeleza jukwaa hili ni kuunga mkono juhudi za Serikali na za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake kiuchumi, kuongeza ushiriki wao katika sekta mbalimbali na kuhamasisha maendeleo jumuishi, ”

Ametaja mafanikio ya Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kijamii na kiuchumi sambamba na hatua kubwa ya kuhakikisha kuwa mwanamke anakuwa sehemu ya maendeleo katika jamii kuwa ni fursa za elimu, mazingira wezeshi ya kiuchumi, ushirikiano na jumuiya ya kimataifa, huduma bora za afya pamoja na huduma za maji safi na nishati ya kupikia.

Aidha, Dkt. Biteko ametoa rai kwa wadau wote muhimu kushirikiana na Serikali ili kutokomeza changamoto zinazohitaji kutatuliwa ili kufungua fursa zaidi kwa wanawake.

Vilevile ametoa wito kwa Clouds media na wanawake kushiriki kikamilifu katika kampeni mbalimbali za Serikali mfano Kampeni ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kuhakikisha wanawake wanatumia Nishati Safi na kuwa na afya salama.

Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufikia malengo tarajiwa.



Prev Post TRA Yakusanya Shilingi Trilioni 7.53 kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025
Next Post Rais Samia Afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook