
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kushika nyadhifa muhimu katika taasisi za umma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo umegusa maeneo mbalimbali ya kiutawala na maendeleo ya kitaifa.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
1. Prof. John Wajanga Aron Kondoro – Amekuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akichukua nafasi ya Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko aliyemaliza muda wake.
2. Prof. Emanuel Amaniel Mjema – Amekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kipindi cha pili.
3. Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo – Amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), akichukua nafasi ya Prof. Esnat Chaggu aliyemaliza muda wake.
4. IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro – Amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), akichukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo aliyemaliza muda wake.
5. Bi. Rosemary William Silaa – Amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kipindi cha pili.
Uteuzi huu unaonesha dhamira ya Rais Samia ya kuendelea kuimarisha taasisi za umma kwa kuwapa nafasi viongozi wenye uzoefu na weledi katika nyanja mbalimbali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!