
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 7.53 kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025, ikizidi lengo la Trilioni 7.43 kwa ufanisi wa asilimia 101.32. Hili ni ongezeko la asilimia 13.47 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita.
Kwa mujibu wa TRA, mafanikio haya ni sehemu ya mwenendo mzuri wa ukusanyaji mapato ambapo kwa kipindi cha miezi tisa (Julai – Machi), mamlaka imekusanya Shilingi Trilioni 24.05, ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.01 kutoka mwaka uliopita. Hili ni kiwango cha juu zaidi kufikiwa katika historia ya mamlaka kwa kipindi kama hiki.
TRA imesema mafanikio haya yanatokana na usimamizi madhubuti wa mifumo ya kodi, uboreshaji wa teknolojia, na ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuhakikisha ulipaji kodi unakuwa endelevu kwa maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!