Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kitima: Nilichofanyiwa na Vyombo vya Dola Sipendi Mwingine Afanyiwe

  • 35
Scroll Down To Discover

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima.

“Vyombo vya dola vimekuja kunihoji, nimewaeleza niliyodhani kwa wakati ule waliyahitaji. Wenyewe wanajua, wanalijua hili tukio vizuri… mbele ya Mungu wanalijua vizuri,” Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima ambaye alikuwa akihojiwa na Chombo kmoja cha Habari ofisini kwake hivi karibuni.

Akafafanua kuwa tukio la yeye kushambuliwa na watu wasiojulikana linafahamika vizuri na vyombo vya dola, na kwamba hatua zaidi kuhusu uchunguzi na haki zipo katika vyombo hivyo vya usalama, amesema kuwa tayari amehojiwa na maofisa wa usalama (polisi) ambao walipata maelezo yake, na sasa anasubiri hatua zao.

Ameeleza kuwa haitakuwa vyema kwa vyombo vya dola kufanya kwa Watanzania wengine kile alichofanyiwa yeye na ameonesha masikitiko yake kuhusu ukimya wa kisheria licha ya tukio hilo kujulikana vema kwa mamlaka husika.

“Nisingependa Mtanzania yeyote vyombo vya dola vinavyolifanyia kazi suala langu wanavyonifanyia mimi wawafanyie wengine hivyo, nisingependa wafanye hivyo kwasababu kama watu wanalijua tukio, na huoni kinachoendelea, nisingependa wengine wakosewe kiasi hicho”, ameeleza Padri Kitima.

Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro lilisema Padri Kitima alishambuliwa na watu wawili wasiojulikana usiku wa Aprili 30, 2025, akiwa njiani kuelekea maliwatoni katika makazi yake yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam. Alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan, ambako alitibiwa na kuruhusiwa baadaye kutoka baada ya kulazwa siku kadhaa.

STORI NA ELVAN SITAMBULI | GPL



Prev Post Miaka 39 Madarakani: Museveni Aidhinishwa Kugombea Tena
Next Post JKT Yahimiza Watanzania Kununua Bidhaa Za Ndani Kwa Maendeleo Ya Taifa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook