Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Miaka 9 ya Maumivu! Said Mrisho Avunja Ukimya! Ali Kiba Alinisaidia Kodi – Video

  • 37
Scroll Down To Discover

Said Mrisho

Ni miaka tisa imepita sasa tangu kutokea kwa tukio lisilo la kawaida, lililozigusa hisia za wengi, tukio la kijana Said Mrisho, kuchomwa visu na kutobolewa macho na kijana mwingine, Salum Njwete almaarufu Scorpion, lililotokea Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam.

Scorpion yupo mtaani baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani alichohukumiwa baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo lakini kwa upande wa Said aliyetobolewa macho, mambo hayajawahi kuwa sawa tena!

Kwenye mahojiano Said amefunguka kuwa ingawa alikuwa anafahamu kuwa ipo siku atakufa kama binadamu wengine, hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku maisha yake yangebadilika ghafla na kuwa mlemavu.

Akaendelea kufunguka kuhusu maisha yake na kueleza kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, ni miongoni mwa watu waliowahi kumsaidia, hasa katika kipindi ambacho alikuwa na changamoto zinazohusu masuala ya kodi.

Tukio la kutobolewa macho, limebadilisha kila kitu kwenye maisha yake na sasa amekuwa ni mtu wa kuomboleza kila siku, mithili ya mtu mwenye msiba mzito.

Hapa anasimulia kuhusu ahadi zilizotolewa kipindi alipopata matatizo na utekelezaji wake.



Prev Post Expanse Tournament, Jiunge, Cheza, na Shinda Zawadi Kubwa kutoka Meridianbet
Next Post Miaka 39 Madarakani: Museveni Aidhinishwa Kugombea Tena
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook