Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Baraza la Maaskofu Lapiga Marufuku Hotuba za Wageni Madhabahuni

  • 43
Scroll Down To Discover

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetangaza mabadiliko ya Liturujia, likiboresha baadhi ya vipengele vya ibada ikiwa ni pamoja na kuondoa rasmi nafasi ya wageni  wakiwemo viongozi wa kiserikali kutoa hotuba, salamu au pongezi ndani ya Kanisa.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TEC, kipengele cha matangazo ambacho awali kiliruhusu wageni kutoa neno, kimefutwa. Mabadiliko haya yanalenga kudumisha utakatifu na mpangilio wa ibada za Kanisa Katoliki.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa:

“Hakutakuwa na hotuba za kupongezana, isipokuwa tu Mwadhimishaji (Paroko/Padri kama ni tukio la Kiparokia, Askofu wa Jimbo kama ni tukio la kijimbo, Rais wa TEC kama ni tukio la kitaifa) atatambua kwa ufupi uwepo wa wageni wa kidini, kiserikali, kijamii na waalikwa wote bila kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia.”

Aidha, imebainishwa kuwa mwadhimishaji mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kuwaalika wageni waliobeba zawadi kutoa sadaka zao, lakini bila ya wao kutoa salamu, pongezi au hotuba yoyote ile.

Uamuzi huu unalenga kuimarisha utaratibu wa ibada na kuheshimu nafasi ya liturujia kama sehemu takatifu ya mawasiliano kati ya Mungu na waamini, bila kuingiliwa na shughuli au matamko yasiyo ya kiibada.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumamosi tarehe 21 June 2025
Next Post Katibu Mkuu wa CCM Atoa Pole kwa Familia ya Marehemu Mobutu Malima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook