Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Familia ya Hayati Edgar Lungu Yapanga Mazishi Afrika Kusini Licha ya Taarifa ya Serikali ya Zambia

  • 42
Scroll Down To Discover

Hayati Edger Lungu

Juni 19, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alitangaza kuwa Rais wa zamani wan chi hiyo Hayati Edger Lungu atazikwa nchini Zambia kwa heshima zote za kiserikali na sio nchi nyingine yoyote, Familia ya Dkt. Edgar Lungu imetangaza kuwa mazishi yake yatafanyika nchini Afrika ya Kusini kwa ibada ya faragha.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Familia hiyo, Makebi Zulu jana Juni 20 imeeleza kuwa nchini ya Afrika ya Kusini imeridhia kuipa familia hiyo uhuru wa kufanya ibada muhimu ya mazishi bila kuwaingilia.

“Kwa niaba ya familia ya Lungu, tunapenda kutangaza kwamba mazishi na ibada ya mwisho ya mpendwa wetu, Dkt. Edgar Chagwa Lungu, yatafanyika hapa Afrika Kusini, kwa mujibu wa matakwa ya familia ya kuwa na ibada ya faragha.” imesema taarifa

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini kwa msaada wao wa heshima na kwa kuheshimu uamuzi wa familia wa kufanya ibada ya faragha hapa Afrika Kusini.” ameongeza Makebi

Hata hivyo taarifa imesema kuwa itaendelea kutafuta mshikamano na amani baina ya Wazambia katika kipindi hiki kigumu huku wakieleza kuwa hivi karibuni itatolewa taarifa juu ya siku ya mazishi na ibada ya mwisho ya Lungu.

IRAN YAIAMBIA ISRAEL KIPIGO KIKUBWA ZAIDI CHAJA- YADAI CHA SASA HAKIJAFIKIA HATA ASILIMIA 30…!



Prev Post Katibu Mkuu wa CCM Atoa Pole kwa Familia ya Marehemu Mobutu Malima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook