Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: Awamu ya Pili Mradi wa Maji Mwanga Same Korogwe Kutekelezwa

  • 25
Scroll Down To Discover

Amempongeza Dr samia kutoa fedha Biloi 400 kutekeleza mradi mkubwa maji.

Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema awamu ya pili ya mradi wa maji wa Same – Korogwe utaanza Hedaru kuelekea Korogwe.

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kutolewa kwa fedha kiasi cha Sh bilioni 400 ili kukwamua mradi wa maji ambao ulikwama kwa muda mrefu.

Makalla ameeleza hayo leo Juni 11 wakati akizungumza na wananchi wa katika eneo la Hedaru Jimbo la Same Magharibi wilayani Same mkoani Kilimanjaro akihitimisha ziara yeke katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Makalla amesema awamu ya pili ya mradi huo utapita katika vijiji 24 kutokea Same Mjini kupita Hedaru na vijiji Vitano vya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Awali Makalla amesema mradi huo wa maji uliwasumbua kwa muda mrefu kwa awamu mbili za uongozi zilizopita lakini chini ya uongozi wa Rais Samia matokeo yameonekana kwa kuidhinisha kutolewa kiasi tajwa cha fedha kukwamua mradi huo.

Makalla amesema mradi wa Mwanga -Same hadi Korogwe ulipata mkandarasi na akawa anasua sua katika utekelezaji akafukuzwa na hadi hapo umetumia jumla ya Sh bilioni 400 katika utekelezaji wake na maji yamefika Same Mjini na Mwanga.



Prev Post Rais Samia Afuatilia Uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025/26 – Video
Next Post Dkt. Nchimbi Akifuatilia Bajeti Kuu Ya Serikali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook