Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

STARS KUKIPIGA NA BAFANA BAFANA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO….

  • 30
Scroll Down To Discover

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo kuikabili timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Peter Mokaba, mjini Polokwane, kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mechi hii ni ya kutengeneza pesa na Meridianbet kwa wabashiri wote.

Ni mchezo wa kirafiki, lakini pande zote mbili zinatarajiwa kuupa uzito mkubwa mchezo huo ili kuutumia kama sehemu ya maandalizi ya michuano ya (COSAFA). Kwa upande wa Tanzania, mchezo huu pia ni fursa muhimu kwa Kocha Mkuu Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea michuano ya CHAN itakayofanyika mwezi Agosti, pamoja na mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi Septemba.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Morocco amesema kuwa pambano dhidi ya Afrika Kusini ni sehemu ya tathmini ya kina ya uwezo wa wachezaji wake, sambamba na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika michezo ya awali.

Kikosi cha Taifa Stars kinaundwa na wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi na nje ya mipaka, akiwemo Simon Msuva anayechezea klabu ya Al Talaba ya Iraq, Selemani Mwalimu wa Wydad AC ya Morocco, pamoja na Alphonce Mabula kutoka klabu ya Shamakhi ya Azerbaijan. Uwepo wao unatazamiwa kuimarisha safu ya timu kwa kuleta uzoefu wa kimataifa, jambo linaloonekana kuwa na umuhimu mkubwa katika mashindano yajayo, yakiwemo yale ya CECAFA. Kwa ubora wa vikosi vyote viwili, Meridianbet imekuwekea machaguo mengi sana ili uchague ubashiri upi utafaa kwako.

Kihistoria, Tanzania na Afrika Kusini zimekutana mara tatu katika mechi za kimataifa. Mwaka 2002 timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, mwaka 2011 Bafana Bafana walishinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki, na mwaka 2017 Taifa Stars walijibu mapigo kwa ushindi wa bao 1-0 katika michuano ya COSAFA.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa na burudani ya kiwango cha juu, huku Taifa Stars ikisaka kuendeleza rekodi nzuri dhidi ya wenyeji wao. Mashabiki wa soka nchini na nje ya mipaka wanahimizwa kuufuatilia mchezo huu kwa ukaribu, na kuweka ubashiri wao mapema kupitia Meridianbet.

The post STARS KUKIPIGA NA BAFANA BAFANA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SAMSUNG A25 NI YAKO UKIBASHIRI NA MERIDIANBET LEO….
Next Post KWA NINI KILA MTU ANA MISTARI TOFAUTI YA MKONO? SIRI YA KIPEKEE INAYOFICHWA NA KIGANJA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook