Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Viongozi wa Dini Wamjia juu Spika kwa Kumtangaza Museveni ‘Mungu’

  • 39
Scroll Down To Discover

Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among

Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wametoa ujumbe wa kumlaani Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among baada ya kusema kuwa Rais Yoweri Museveni ni Mungu na kumwita mwanae mwana wa Mungu.

Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti kuwa kumtaja Rais Museveni kuwa ni Mungu kumewakasirisha baadhi ya viongozi wa kidini wanaosema ni kufuru.

Gazeti la Daily Monitor linaripoti kwamba bunge la Uganda limejibu kwa kusema kwamba matamshi ya Anita yalikuwa “mfano tu kwa madhumuni ya maelezo”.

Siku ya Jumapili, Anita Among alikuwa akiwafanyia kampeni wabunge wa chama tawala cha NRM katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Januari Mosi mwaka ujao.

Rais Yoweri Museveni ni Mungu

Hivi majuzi Anita alitangaza kuwa anataka kubaki katika nafasi yake kwa muhula mwingine kuanzia 2026–2031, ambao alisema utakuwa wa mwisho katika nafasi hiyo ambayo ameshikilia tangu 2022.

Akiwa Kyazanga, kilomita 50 kusini mwa mji wa Masaka, Anita Among alipiga magoti na kuwaomba watu wa eneo hilo kuwapigia kura wabunge wa chama cha NRM aliowateua, akisema: “Napiga magoti, namuunga mkono Rais Museveni” na wagombea wa NRM. Kisha akasimama.

Katika video hiyo iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, Anita aliongeza: “Kama nilivyowaambia mara ya mwisho, sisi katika Teso [eneo lililo mashariki mwa Uganda] tunaamini Utatu Mtakatifu. Tunaamini katika Mungu Baba, na Mungu Baba ni Rais Museveni, [anarudia] Mungu Baba ni Rais Museveni. Mungu Mwana ni MK [Muhoozi Kainerugaba], sasa nyinyi mko katika Roho Mtakatifu, kwa hiyo muwachague.

Stori: Elvan Stambuli, GPL



Prev Post Msigwa Atoa Onyo Kuhusu Matumizi Mabaya ya Mitandao ya Kijamii – Video
Next Post Musukuma Awavunja Mbavu Bungeni – ”Kunitenganisha Mimi Na Mke Wangu Ni Kukiuka Maadili Ya Ndoa” – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook