

Wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Zanzibar na makamu mwenyekiti mstaafu wa chama hicho wamefungua kesi Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam wakilalamikia mgawanyo wa rasilimali za chama usio sawa kati ya Bara na Zanzibar na upendeleo na ubaguzi. Chama Cha Demokrasia na Maenendeleo (Chadema) kiliweka pingamizi kesi itupwe lakini Mahakama imewakatalia hivyo kesi hiyo itasikilizwa Juni 24, 2025 Mahakamani hapo.

Akizumgumza na waandishi wa habari mapema leo, 12 Juni, 2025 jijini Dar-es-Salaam, Gido Thomas Simfukwe amesema kuwa katika kesi ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ya mgogoro wa mgawanyo rasilimali dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametaka Umma usipotoshwe katika zuio la Mahakama kwa Chama hicho kutofanya shughuli za kisiasa.
“Taarifa ambazo zinazosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii za kwamba Chadema inatakiwa kusitisha shuguli zake kwa siku 14 ni za upotoshaji na ufafanuzi kuhusu kufungiwa kwa chama ni kwamba Mahakama haikusema siku 14, Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, Hamidu Mwanga katika uamuzi wake alisema anazuia shughuli za Chadema za kisiasa hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa,” amesema Simfukwe.
Simfukwe akifafanua hilo amesema, “Kesi ya msingi inasikilizwa Juni 24, 2025 na Mahakama haikusema imezuia kwa siku 14 huo ni upotoshaji,”.
Aidha amesema kuwa uamuzi wa pili Mahakama imeagiza Chadema, Bodi ya wadhamini na katibu mkuu kwamba mali zote za Chadema zisitumike mpaka pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kila upande utabeba gharama zake ambapo kesi hiyo ya msingi itasikilizwa Mahakamani hapo Juni 24, 2025
ReplyForward
|
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!