MAGAZETI ya Leo Jumatano 07 May 2025
Taarifa za uhakika ni kuwa Simba iko katika mchakato wa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum ‘Fei Toto’
Inaelezwa kuwa juzi Rais wa heshima wa Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ alifanya mazungumzo na Wawakilishi wa Fei Toto ambapo kimsingi ‘tajiri‘ amempa Fei ofa nono ya mshahara na dau la usajili
Hatua iliyobaki ni kukamilisha mazungumzo na Azam Fc ambayo bado inamkataba wa mwaka mmoja na Fei Toto ambaye alijiunga na timu hiyo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga
Simba ina uhakika wa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao na malengo ni kufanya vyema kama walivyofanya msimu huu katika michuano ya kombe la Shirikisho Simba ikitinga fainali ambapo itacheza na RS Berkane
Fei Toto amekuwa ‘injini’ ya Azam Fc katika misimu miwili akifunga mabao 23 na kutoa pasi 21 za mabao
Jean Charles Ahoua ndiye tegemeo katika la kiungo cha ushambuliaji cha Simba lakini ni wazi imeonekana eneo hilo linahitaji kuongezewa nguvu, Fei Toto ndiye kiungo bora wa ushambuliaji kwa sasa katika ligi kuu ya Tanzania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!