
Msafara wa baiskeli wa Twende Butiama Cycling Tour 2025 umeanza rasmi Julai 3, 2025, ukiwana waendesha baiskeli zaidi ya 180 wakiwa njiani kuelekea Butiama. Safari hii ya kihistoria, yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,500 na inayotarajiwa kuchukua takribani siku 11, inalengakumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere, kwa kuendeleza mapambano dhidi yamaadui watatu ambao ni Ujinga, Umasikini na Maradhi hapa nchini. Ukidhmainiwa na Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania, msafara huu umeanzia jijini Dar es Salaam na kwa siku 11 unategemewa kupita katika mikoa 11, ukibeba ujumbe wa matumainina mabadiliko chanya.

Njiani, msafara huu unatoa huduma mbalimbali zenye kugusa maisha ya wananchi moja kwamoja. Hizi ni pamoja na kampeni kubwa za upandaji miti zinazolenga kupanda miti 50,000 ilikulinda mazingira, na kutoa msaada muhimu wa elimu kwa shule mbalimbali. Msaada huu waelimu unajumuisha ugawaji wa madawati 1,500 kwa shule 10 za msingi pamoja na baiskeli 50 kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule (hasa wasichana), ili kuwawezesha kufika shuleni kwaurahisi. Waendesha baiskeli wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali za Afrika na hata Marekani naUlaya wamejiunga na msafara huu, wakionesha ushirikiano wa kimataifa katika kuletamaendeleo.
Msafara wa huu unatarajiwa kufika Butiama tarehe 13 Julai, 2025, ukiacha kumbukumbu yakudumu katika jamii nyingi zilizofikiwa. Lengo kuu la waandaaji ni kuwafikia Watanzania zaidiya 700,000, wakiwemo watoto, vijana na wazee, na kuendeleza urithi wa Mwalimu Nyerere wakupambana na ujinga, maradhi na umasikini. Kampeni hii inaendelea kudhihirisha nguvu yaushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuleta mabadiliko chanya na endelevu kwamustakabali bora wa Tanzania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!