Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo ametembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Omolo ameipongeza PPAA kwa kuanza matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST. Kupitia maonesho hayo, Bi. Omolo amefahamishwa majukumu na mafanikio ya Mamlaka ya Rufani kwa kipindi cha miaka minne chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!