Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwenyekiti wa CHADEMA Iringa Mjini, Frank Nyalusi Afariki

  • 41
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Ijumaa Septemba 19, 2025, katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa mapema leo na viongozi wa chama hicho, wakieleza kuwa kwa sasa wanasubiri taratibu za kifamilia kabla ya kutangaza rasmi ratiba ya mazishi.

Marehemu Nyalusi aliwahi kujitokeza mwaka 2020 akiwania kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia CHADEMA, ambapo katika kura za maoni aliishia nafasi ya tatu.

Kifo chake kimeacha simanzi kwa familia, ndugu, marafiki pamoja na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wakimtegemea katika safari ya kisiasa ndani ya chama hicho.

TAARIFA ya POLISI KUHUSU MWANAFUNZI wa CHUO cha MZUMBE ALIYETEKWA na KUKUTWA AMEUAWA na KUCHOMWA….



Prev Post Miili ya Masista waliofariki ajali ya gari yawasili Dar – Video
Next Post Ubia Serikali na Sekta Binafsi Nguzo Kuu ya Dira 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook