
NAFASI Za Kazi Tarime Town Council
NAFASI Za Kazi Tarime Town Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime anayofuraha kuwatangazia nafasi Nne (04) za kazi katika Ajira ya kudumu kwa Watanzania wote wenye sifa stahiki baada yankupokea Kibali cha Ajira mpya kwa Mwaka 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
MPISHI DARAJA LA II NAFASI MBILI (02)
KAZI NA MAJUKUMU:
- Kusafisha jiko.
- Kupika chakula cha kawaida.
- Kupika vyakula vya aina mbalimbali.
- Kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula viko safi.
- Kusafisha maeneo ya kupikia.
SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha IV.
- Awe amefuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya ‘Food Production’ yatolewayo na vyuo vya forodhani (Dar es Salaam), Masoka (Moshi), Arusha Hotel, VETA (Mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara wa Serikali Mpishi Daraja la II ataanza na TGS C kwa mwezi.
DEREVA DARAJA LA II NAFASI MBILI (02)
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hari ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mabilimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari na
- Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na msimamizi wake
SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha IV.
- Awe na leseni ya udereva ya Daraja la “C” au “E” ya uendeshaji Magari ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali, pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving C ourse) yatolewayo na chuo cha VETA au NITau chuo kingine kinachotambuliwa
na serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara wa Serikali Dereva Daraja la II ataanza na TGS B kwa mwezi
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
- Mwomabaji awe hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote la jinai.
- Waombaji wote waambatanishe nakala za vyeti vya taaluma, nakala ya cheti cha kidato cha Nne/Sita, zilizothibitishwa na Hakimu au Wakili aliyetambulika na Serikali.
- Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa iliyothibitishwa na Hakimu au Wakili anayetambulika na Serikali.
- Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini (Referees) watatu na picha moja ya passport size ya hivi karibuni (iandikwe majina kamili kwa nyuma). - Testimonials, Provisional Results Slips, Statements of results,Hati za Matokeo za kidato cha nne na Sita (Form IV na VI Results Slips) na Transcripts ambayo haikuambatanishwa na cheti havitakubaliwa.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi
- ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA au NACTE).
- Waombaji ambao ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliopo katika Utumishi wa Umma wasiombe nafasi hizi.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa sababu yeyote ile hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
- Waombaji watakaowasilisha vyeti na taarifa za kugushi watachukuliwa hatua kali za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
- Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja II wenye Leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo vya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
Waombaji wote waambatanishe nakala ya Kitambulisho cha NIDA au Namba ya utambulisho wa Uraia (National Identification Number) kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji,
S.L.P 45,
TARIME
Maombi yatumwe kupitia mfumo wa Ajira Portal Tovuti www.ajira.go.tz
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 11/08/2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!