Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto ashangazwa na Mataifa ya Nje kuingilia mambo ya Ndani Afrika

  • 44
Scroll Down To Discover

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimestushwa na baadhi ya Taasisi na Mashrika ya Nje kuhoji kwa vitisho kukamatwa baadhi ya Wanasiasa wanaovunja Sheria wakati Nelson Mandela wa Afrika Kusini na wenzake wamekaa jela miaka 27 bila Mashirika hayo kuhoji .

Pia chama hicho kimesikitishwa na utamaduni mpya wa Mataifa ya Nje kuingilia Mambo ya Ndani ya Serikali za Afrika.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis, amesema ikiwa Afrika haiingilii mambo ya ndani ya Mataifa mengine ,ni makosa Afrika kupangiwa hatma yake na mataifa ya kigeni.

Mbeto alisema ni lazima na shuruti muhimu kwa Mataifa ya Afrika, kuutafakari mwenendo huo mzima ambao kimsingi , hautoi nafasi kwa Serikali za kiafrika kutumia uhuru wake wa kujiamua mambo yake yenyewe .

Alisema tabia hiyo inakwenda kinyume na taratibu za msingi , Kanuni , Miiko adilifu ya Diplomasia pia ni ukiukaji mkubwa wa Mikataba Kimataifa.

“Kudumisha mahusiano na ushirikiano wa Kimataifa ni jukumu litakaloifanya dunia kuwa eneo salama. Yanapotumika mabavu na vitisho badala ya kuendeleaza mahusiano mema hayo huwa maonevu ya kifikra na Ukoloni Mamboleo” Alisema Mbeto

Aidha, Katibu huyo Mwenezi alisema Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini walipopinga Siasa za ubaguzi wa rangi , walifikishwa Mahakamani na kutupwa magerezani kinyume na haki, hakuna nchi yoyote Nje ya Afrika iliolaani maonevu hayo.

“Wananchi wa Namibia, Msumbiji , Angola ,Cape Verde , Zimbabwe na Afrika Kusini walinyanyasika . Hakuna aliyewatetea zaidi ya Waafrika wenzao .Ni ajabu wakandamizaji haki wa zamani wanataka kujikosha ili wajionyeshe kuwa watetezi wa batili” Alisema Mwenezi huyo .

Pia Mbeto alionekana kushangazwa kuona baadhi ya Wanasiasa wa Upinzani Barani Afrika wakifanya Siasa za shari , uvunjaji wa sheria huku wakitegemea kupata nguvu ya utetezi toka kwa Mataifa ya kigeni .

‘Lazima Viongozi wa Afrika waanze kujadili kuibuka kwa utamaduni wa kejeli na kuweka Azimio na msimamo wa pamoja . Haiwezekani watesaji wa zamani, jana na juzi leo wageuke na kuwa watetezi wa haki” Alieleza.

Hata hivyo, Katibu huyo Mwenezi alisema Afrika impoteza viongozi wake kadhaa kina Patrice Lumumba (DRC) , Abeid Karume (Zanzibar), Thomas Sankara (Bukinafaso) Murtala Mohamed (Nigeria) na Marian Ngwabi (Kongo Brazaville) kwa njama toka nje ya Afrika .



Prev Post Zelensky: Tunafanya Mazungumzo Na Trump Kuhusu Mpango Wa Ndege Zisizo Na Rubani
Next Post Rais Mstaafu JK Ampongeza Rais Samia Kwa Dira 2050 Na Uongozi Mahiri – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook