Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Bodi ya Ithibati Yawafungia Watangazaji wa Mjini FM kwa Ukiukwaji wa Maadili

  • 8
Scroll Down To Discover

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari nchini imetoa agizo la kuwasimamisha watangazaji watatu wa Kipindi cha Genge kinachorushwa na kituo cha Mjini FM, wakituhumiwa kukiuka maadili ya taaluma ya habari pamoja na kukosa sifa za kitaaluma zinazohitajika kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Patrick Kipangula, watangazaji waliosimamishwa ni Crispin Mgenge, Perfect Crispin, na Iddy Bakari. Bodi imesema kuwa marufuku hiyo itadumu kuanzia Julai 18, 2025, hadi pale watakapokidhi matakwa ya kisheria, yakiwemo ya kuwa na elimu stahiki na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mahojiano yao na msanii wa muziki wa Singeli, Dogo Paten, kuzua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kutokana na maudhui yaliyotajwa kuwa ya kudhalilisha, yenye lugha isiyofaa, na kinyume na maadili ya kitaaluma.

Bodi imeeleza kuwa, katika kipindi hicho, watangazaji hao:

Hawajasajiliwa na kupewa ithibati na Bodi kama sheria inavyotaka,

Walikiuka haki ya faragha ya mhojiwa kwa kumlazimisha kutoa taarifa binafsi bila ridhaa yake,

Walitumia lugha ya kumshushia hadhi mhojiwa, kinyume na kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maamuzi hayo yalitokana na tathmini ya kitaaluma na mahojiano maalum yaliyofanywa kati ya Bodi na watangazaji husika kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi.

Bodi imesisitiza kuwa hatua hizi ni sehemu ya juhudi za kulinda hadhi ya taaluma ya habari nchini na kuhakikisha maudhui yanayotangazwa yanazingatia misingi ya kimaadili, kitaaluma na kisheria.



Prev Post Fursa ya Kukodisha Hoteli ya Kisasa – NSSF Mafao House Mwanza
Next Post TLS Yapinga Ufafanuzi wa Zuio la Mahakama Dhidi ya Viongozi wa CHADEMA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook