Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mgombea mwenza wa CCM, Dkt. Nchimbi, apiga kambi Kagera kusaka kura za kishindo

  • 3
Scroll Down To Discover

MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili katika uwanja wa Kashai,Bukoba mjini kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni lSeptemba 7, 2025 mkoani Kagera.

Awali leo Dkt.Nchimbi ameanza ziara yake ya kampeni Mkoani humo akianzia Jimbo la Ngara, Kyerwa, Katoro-Bukoba Vijijini na kuhitimisha kwa mkutano mkubwa jioni hii hapa Bukoba Mjini.

Dk Nchimbi anaendele na mikutano yake ya kampeni ya kusaka kula za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima,ambapo kwa sasa yuko mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo alianzia mkoani Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita na sasa yupo mkoani Kagera.

Dkt.Nchimbi anaendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akimsikiliza Mlemavu wa Miguu,Amos Kalungula mara baada ya kuwahutibia Wananchi wa Bukoba Mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashai, leo Jumapili Septemba 7, 2025 mkoani Kagera.

 

 



Prev Post Wananchi Kome Wampokea Shigongo Kwa Shangwe, Aahidi Mshikamano
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook