Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Puma Energy Yazindua Kampeni Ya Twende Tanzania Na Safari Ya Uhakika Na Oil Za Puma

  • 9
Scroll Down To Discover

Kampuni ya Puma Energy Tanzania leo imezindua rasmi kampeni kabambe ya promosheni kwa wateja wake kwa jina la “Twende Tanzania na Safari ya Uhakika na Oil za Puma”, itakayodumu hadi Oktoba mwaka huu, ambapo mshindi mkuu atajishindia mafuta yenye thamani ya shilingi milioni 5, atakayoweza kuyatumia kwa mwaka mzima kupitia kadi maalum.
Akizungumza na wanahabari mapema Leo, Julai, 18,2025 jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Bi. Lilian Kanora, amesema kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kutoa shukrani kwa wateja wake wanaoendelea kutumia bidhaa na huduma za Puma kote nchini.
“Puma ndiyo Kampuni namba moja ya mafuta Tanzania. Kupitia kampeni hii, tumeamua kuwazawadia wateja wetu kwa uaminifu wao kwa kuwapa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na mafuta ya bure kwa mwaka mzima,”
Pia ameeleza kuwa kampeni hiyo itahusisha wateja wanaonunua mafuta na bidhaa za oil katika zaidi ya vituo 90 vya Puma Energy vilivyopo nchini kote. Wateja wataweza kujishindia zawadi ya shilingi 200,000 kila mmoja, huku mshindi wa jumla akipokea zawadi ya mafuta ya shilingi milioni 5 kupitia kadi maalum atakayotumia kwa mwaka mzima katika vituo vyote vya Puma Energy Tanzania.
“Kwa mshindi wa kwanza, atakuwa na kadi maalum ya kuweka mafuta kwenye vituo vyetu bila malipo kwa mwaka mzima. Washindi wengine wa zawadi ya 200,000 wataweza kununua bidhaa mbalimbali katika maduka yetu ya Puma, amesema Bi.Kanora.
Nae Bw. Prosper Kasenegala, ambaye pia ni mwakilishi wa Puma Energy, alizungumza kuhusu bidhaa mpya ya oil iliyoletwa na kampuni hiyo ambayo inamwezesha mteja kufanya huduma za gari kwa unafuu mkubwa.
“Oil zetu mpya za Puma zimeboreshwa ili kumpunguzia mteja gharama za huduma. Kama awali ulilazimika kubadilisha oil kila baada ya miezi miwili, sasa kwa kutumia oil za Puma utaweza kubadilisha baada ya miezi minne – jambo ambalo ni nafuu kubwa kwa wateja wetu,” amesema Bw. Kasenegala.
Aidha amesema kuwa Puma Energy pia imejikita katika kutoa elimu na ushauri kwa wateja wake kuhusu matumizi sahihi ya oil na aina sahihi ya kiambatanishi kinachopaswa kutumika kulingana na kifaa au chombo cha mteja husika, ikiwa ni sehemu ya dhamira yao ya kuhakikisha usalama na ufanisi wa vyombo vya wateja



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 14, 2025
Next Post Fursa ya Kukodisha Hoteli ya Kisasa – NSSF Mafao House Mwanza
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook