Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JKT Yahimiza Watanzania Kununua Bidhaa Za Ndani Kwa Maendeleo Ya Taifa

  • 33
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele, ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwa kutumia malighafi za ndani, akisisitiza kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya kuongeza tija ya uzalishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Meja Jenerali Mabele alisema kuwa jukumu la kukuza bidhaa za ndani halipaswi kubaki mikononi mwa serikali pekee, bali ni la kila Mtanzania mmoja mmoja.

“Ni lazima tuamini katika uwezo wetu. Tunavyozalisha fanicha bora kwa kutumia rasilimali za hapa nyumbani, ni muhimu jamii nayo ione thamani ya kuvitumia,” alisema Meja Jenerali Mabele.

Katika maonesho hayo, JKT walitunukiwa tuzo ya uzalishaji bora wa fanicha na ubunifu wa ndani, kama sehemu ya kutambua mchango wao kwenye sekta ya viwanda vidogo na vya kati.

Kwa mujibu wa Mabele, JKT imekuwa mshiriki wa kudumu wa maonesho hayo kwa miaka mingi, na mwaka huu walionyesha bidhaa mbalimbali zikiwemo:

Fanicha za ndani na ofisini

Vifaa vya matumizi ya majumbani

Huduma za ulinzi
Zote zikiwa zimebuniwa na kutengenezwa na vijana wa JKT kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.

Amesisitiza kuwa kuunga mkono bidhaa hizi kunamaanisha kuunga mkono ajira kwa vijana, kukuza teknolojia ya ndani, na kuimarisha uchumi wa Taifa kupitia matumizi ya rasilimali asilia za Tanzania.

SAID ALIYETOBOLEWA MACHO na SCORPION AFUNGUKA MAZITO MAPYA – MAGUMU ANAYOPITIA… | MAPITO



Prev Post Kitima: Nilichofanyiwa na Vyombo vya Dola Sipendi Mwingine Afanyiwe
Next Post DIB YAENDELEA KUELIMISHA UMMA KUHUSU MAJUKUMU YAKE KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook