Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yachukua Hatua Dhidi ya “Cutting Master” kwa Kuwahusisha Watoto Katika Maudhui ya Kingono

  • 45
Scroll Down To Discover

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu imetangaza hatua kali dhidi ya kijana anayefahamika kwa jina la “Cutting Master” kutokana na video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonyesha akiwauliza watoto maswali yenye maudhui ya kingono.

Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema tayari amewasiliana na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Kinondoni kuagiza timu ya wataalamu kufuatilia na kuchunguza kwa kina shughuli za kijana huyo, anayesemekana kuwa na ofisi katika eneo la Mwenge, Dar es Salaam.

“Nimepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kinyozi huyo, anayetuhumiwa kuwahusisha watoto katika maudhui yasiyofaa na kuyasambaza kwenye mitandao. Hili ni kosa kubwa linalokiuka Sheria ya Mtoto Sura ya 13 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao Sura ya 443,” amesema Dkt. Gwajima.

 



Prev Post Rais Samia Aongoza Ufunguzi wa Kanisa Jipya la Arise and Shine, Kawe (Picha +Video)
Next Post Infinix Hot 60 Pro+ Inakuja na Wembamba wa 5.59mm, Kuweka Rekodi ya Kipekee
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook