Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vodacom na Stanbic Wazindua Jezi Itakayotumika Kwenye Msafara wa Twende Butiama 2025

  • 30
Scroll Down To Discover

Kampuni ya Vodacom Tanzania ikishirikana na Benki ya Stanbic imezindua jezi ambayo itatumika kwenye msafara wa Twende Butiama ya 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, amesema kuwa wameungana na Benki hiyo ili kuweza kufanikisha kampeni hiyo ya Twende Butiama ambayo ni ziara ya waendesha baiskeli Nchini,inayolenga kuchochea maendeleo ya kijamii Katika sekta za Elimu, Afya na Mazingira.

“Katika kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo ndio maana sisi Vodacom Tanzania tunaungana na kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo Afya, Elimu na utunzaji wa Mazingira”amesema Besiimire.

Akizungumza mwakilishi kutoka Stanbic Banki Wilmot Ishengoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic Benki,Manzi Rwegasira amesema kuwa na wao wameungana katika ziara hiyo kwa kuchangia milioni Mia Moja kila mwaka ili kufanikisha zoezi hilo.

“Tanzania ni nyumbani maendeleo na ukuwaji wake ni juu yetu katika kupinga maadui watatu ambao ni ujinga umaskini na maradhi hivyo basi kwa kuzingatia hilo tukaguswa na huu msafara tuliona mwaka Jana mafanikio makubwa ambayo yalipatikana kwa jamii tukahamasika kuendelea hivyo basi mwaka huu tupo na mwakani na mwaka unaofuata na tutachangia shilingi milioni mia Moja kwa kila mwaka katika kuendesha shughuli hiyo, amesema.

Kauli mbiu ya msafara wa Twende Butiama 2025 ni Kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni Ujinga, umaskini na Maradhi.ambapo kwa mwaka huu washiriki kutoka Nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi, Congo, Zambia,Malawi, Nigeria pamoja na Marekani watakuwepo.

The post Vodacom na Stanbic Wazindua Jezi Itakayotumika Kwenye Msafara wa Twende Butiama 2025 appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Trump asema amepata mnunuzi wa TikTok
Next Post KIMKAKATI…..HIVI NDIVYO SIMBA ALIVYOCHANGIA KWA 100% YANGA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU..
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook