

Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MNUAT) kimetangaza jumla ya nafasi 54 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya upanuzi wa taasisi na kuanzishwa kwa programu mpya za masomo kuanzia mwaka wa masomo 2026/2027.
Tangazo hilo limetolewa rasmi Desemba 8, 2025, na linalenga kuimarisha rasilimali watu katika kada za taaluma na mafunzo.
Soma zaidi hapa >>>>TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU CHA KILIMO NA TEKNOLOJIA CHA MWALIMU NYERERE (MNUAT)
Nafasi Zilizotangazwa
Ajira hizo zinahusisha nafasi za:
-
Assistant Lecturer (Mhadhiri Msaidizi)
-
Tutorial Assistant (Msaidizi wa Mafunzo)
katika fani mbalimbali ikiwemo:
-
Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji
-
Misitu (Forestry)
-
Ujasiriamali
-
Sayansi na Teknolojia ya Chakula
-
Uhandisi wa Rasilimali za Maji
-
Mitaala na Ufundishaji
-
Zoolojia
-
Usimamizi wa Maliasili
-
Fedha, Benki na Uwekezaji
-
Ikolojia ya Nyanda za Malisho
-
Bustani (Horticulture)
-
Uhifadhi wa Wanyamapori
-
Utalii
-
Ufugaji Nyuki
-
Uhandisi wa Kilimo, Umwagiliaji na Post-Harvest
Sifa za Waombaji
-
Awe Raia wa Tanzania
-
Umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa waliopo kwenye Utumishi wa Umma)
-
Kiwango cha GPA cha juu (3.8 – 4.0 kulingana na nafasi)
-
Waombaji wa Assistant Lecturer wanatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili
-
Waombaji wa Tutorial Assistant wanatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza
-
Kwa Shahada zisizo na GPA, machapisho mawili (2) ya kitaaluma yanahitajika
Soma zaidi hapa >>>>TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU CHA KILIMO NA TEKNOLOJIA CHA MWALIMU NYERERE (MNUAT)
The post MNUAT Yatangaza Ajira Mpya 54, Mwisho wa Maombi Disemba 21, 2025 appeared first on Global Publishers.










Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!