Rais wa Marekani, Donald Trump amesema amepata wa kuinunua kampuni ya TikTok.
Akizungumza kwenye mahojiano na Fox News, Trump amesema kuwa ataweka wazi majina ya wanunuzi hao wiki zijazo huku akisema kuwa ni kundi la watu matajiri sana.
Kauli hiyo inakuja wakati ambapo kampuni ya ByteDance ya China inakabiliwa na shinikizo la kuiuza TikTok kwa Marekani, vinginevyo itazuiwa kutumika nchini humo.
Hata hivyo, Trump amekiri kuwa huenda ikahitajika idhini kutoka kwa nchi ya China kwa ajili ya mauzo hayo, akisema kuwa “Nadhani Rais Xi Jinping ataidhinisha hilo.”
The post Trump asema amepata mnunuzi wa TikTok appeared first on SwahiliTimes.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!