Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Gen Z Warejea Mitaani Kenya Wapaza Sauti Upya Dhidi ya Ukatili wa Polisi

  • 29
Scroll Down To Discover

Maandamano makubwa ya vijana maarufu kama Gen Z, yanatarajiwa leo Jumatano nchini Kenya, mwaka mmoja kamili baada ya maelfu ya waandamanaji tarehe kama ya leo mwaka 2024 kuvamia majengo ya bunge kupinga mswada tata wa fedha, uliokuwa umependekeza nyongeza ya kodi.

Waandaji wa maandamano haya wanasema, yatatumiwa pia, kuwakumbuka watu zaidi ya 60 waliouawa na wengine kujeruhiwa katika maandamano huyo, huku mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani, wakitoa wito kwa polisi, kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, David Maraga aamejiunga katika maandamano hayo ya vijana wa Gen Z jijini Nairobi akilaani ukatili wa polisi dhidi ya vijana.

Francis Auma ni mmoja wa wanaharakati, anyeshiriki kwenye maandamano ya leo, amesema: “Kuna mgawanyiko ndani ya polisi ndio maana unaona hawaelewani yaani ni kama siasa imeingia ndani ya polisi. ” amesema.
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, amewaonya waandamanaji kutovamia majengo ya serikali, ikiwemo ikulu.

‘‘Ni muhimu kutambua kuwa watu, wasiohitajika, hawapaswi kwenda katika maeneo, yaliyoridhiwa kisheria kuwa yanalindwa…tunawaomba waandamanaji waache vitendo vya kuwadhalilisha au kuwakasirisha polisi wakati wanapotekeleza majukumu yao. ’’ Alisema Inspekta Jenerali wa Polisi Kanja.

Kuanzia alfajiri leo Jumatano, maafisa wa usalama wanaopambana na ghasia wameshudiwa kwenye barabara kadhaa za jiji la Nairobi, katika kile kinachoonekana kuwadhibiti waandamanaji.

Stori na Elvan Stambuli | GPL



Prev Post TAMASHA JIPYA LA FILAMU LAJA KILIMANJARO
Next Post Majaliwa Azindua Mitambo Ya Shillingi Billioni 12.4 Kwa Ajili Ya Wachimbaji Wadogo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook