Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu Wa Rais Dkt. Mpango Ashiriki Dominika Ya Ekaristi Takatifu Nchini Italia

  • 39
Scroll Down To Discover

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, akiambatana na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango, wameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka kote duniani kushiriki Dominika ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohana wa Laterano lililopo Roma, Italia.

Ibada hiyo takatifu imeongozwa na Baba Mtakatifu – Papa Leo XIV, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kiimani ya Kanisa Katoliki Duniani.

Makamu wa Rais yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na mikutano mbalimbali ya uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Italia.

 



Prev Post Jeshi La Iran: Marekani Na Israel Zisubiri Majibu Ya Majuto
Next Post Bei ya mafuta ghafi yapanda baada ya Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook