
Kijana Eliya Shilinde, mkazi wa Chanika Dampo jijini Dar es Salaam, ameendelea kuwaomba Watanzania waendelee kumchangia ili apate matibabu ya ngozi yake, ambayo ilibadilika na kuwa nyeupe baada ya kutumia dawa ya antibiotiki iliyokuwa imeisha muda wake.
Eliya anahitaji milioni 40 kwa ajili ya matibabu, lakini hadi sasa tayari amepokea milioni 9 kutoka kwa wahisani. Anasema ana matumaini makubwa kuwa ngozi yake inaweza kurudi katika hali ya kawaida na kuendelea na maisha ya kujenga taifa.
“Mimi siyo Albino. Nateseka sana. Naomba msaada wenu, Watanzania,” amesema Eliya.
Kwa yeyote anayetaka kusaidia, anaweza kuwasiliana kupitia namba: 0762 888 748 – Eliya Shilinde.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!