Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Majaliwa: Rais Dkt. Samia Amedhamiria Kuiendeleza Sekta Ya Madini

  • 4
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa uzinduzi wa kiwanda cha kwanza cha kisasa cha kuchenjua shaba ni ishara ya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuisimamia na kuendeleza sekta ya madini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchenjua tani 31,200 za mashapo ya shaba kwa mwezi kitaleta manufaa kwa Wana-chunya na Taifa kwa ujumla.

Amesema hayo Juni 18, 2025 alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia katika uzinduzi wa kiwanda cha Mineral Access Systems Tanzania Ltd (MAST), kilichopo katika kata ya Mbugani, Chunya mkoani Mbeya.

“Uthubutu na ubunifu wa Rais wetu Dkt. Samia ndio uliochagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo katika Sekta ya Madini, wawekezaji hawa wamekuja kwasababu ya mazingira mazuri ya uwekezaji”.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Wizara ya Madini na Taasisi mbalimbali nchini ziendelee kusimamia wawekezaji ili wanapofanya shughuli zao wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi ikiwemo kulipa kodi stahiki, kutunza mazingira katika maeneo wanapofanya shughuli zao. “Hakikisheni pia wanzingatia Usalama wa wafanyakazi na raia wanaozunguka maeneo ya uwekezaji”.

“Ninyi pia wamiliki wa viwanda na wawekezaji wote hakikisheni mnaendesha shughuli zenu kwa kuzingatia matakwa ya sheria na hasa kwenye utunzaji wa mazingira mkishirikiana na halmashauri wenyeji, kijiji na Wilaya”.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wawekezaji kuweka kipaumbele cha ajira kwa wakazi wanaozunguka maeneo ya uwekezaji ikiwemo za kitaalamu na hata ambazo sio za kitaalamu.

“Ametuambia mkurugenzi mtendaji ameanza na vijana takribani 200 lakini wapo pia ambao wanakuja kila siku na tunaamini atapanua wigo kuajiri, tunataka kuona vijana wa Chunya wakifanya kazi hapa”.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ni sehemu ya utekelezaji wa sera na sheria ya madini inayotaka kuhakikisha madini ya Tanzania yanachimbwa, yanachakatwa na yanaongezwa hapa hapa nchini kabla ya kuuzwa nje ili kupanua wigo wa fursa za kiuchumi.



Prev Post Majaliwa: Rais Dkt. Samia Amedhamiria Kuiendeleza Sekta Ya Madini
Next Post Israel Yashambulia Tena Vituo Muhimu Vya Nyuklia Vya Iran
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook