
Msichana mmoja anayeitwa Teddy, mkazi wa Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, anapitia kipindi kigumu cha kumuuguza baba yake mzazi ambaye ana tatizo kubwa la kiafya.
Upande mmoja wa jicho la baba huyo umelika kabisa na kuwa na kidonda kikubwa kinachotoa wadudu, hali inayosababisha maumivu makali na taharuki.
Kutokana na hali ngumu ya maisha na ukosefu wa fedha, Teddy hulazimika kumtunza na kumsafisha baba yake mwenyewe nyumbani, bila msaada wowote wa kitabibu.
Kwa sasa, wanahitaji kiasi cha Tsh 500,000 kwa ajili ya kufanya vipimo muhimu ikiwemo T-SCAN, vitakavyomwezesha kuanza tiba ya mionzi katika Hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Teddy amewaangukia Watanzania wenzake na watu wenye mapenzi mema kumsaidia ili kuokoa maisha ya baba yake. Kama umeguswa na hali hii, tafadhali changia chochote kupitia namba:
0756 194 166 – Frank Anthony Lingwetu
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!