
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inaendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kutoa huduma bora za matibabu ya kibingwa na kibobezi kwa watanzania na raia wa nchi jirani.
1. Katika kipindi cha Februari hadi Mei 2025, Jumla ya wagonjwa 77,149 wamehudumiwa katika Taasisi ya MOI ambapo wagonjwa wa nje (OPD) walikua 73,887, wagonjwa wa ndani (waliolazwa) walikua 3,262.
2. Katika kipindi tajwa jumla ya wagonjwa 2,330 walifanyiwa upasuaji wa kibingwa na kibobezi, wagonjwa 984 walifanyiwa upasuaji wa dharura na wagonjwa 2,046 walifanyiwa upasuaji wa kawaida.
3. Idadi ya wagonjwa waliofanyiwa uchunguzi wa mionzi (Radiolojia):
Katika kipindi hicho, jumla ya wagonjwa 28, 030 walifanyiwa uchunguzi wa mionzi kama vile X-ray, CT-scan, MRI na huduma nyingine za radiolojia.
4. Pia, katika kipindi hicho, jumla ya wagonjwa 26 wamefanyiwa upasuaji na uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu katika maabara ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suit)
5. Vilevile jumla ya wagonjwa 1,299 wamepata huduma katika kliniki ya MOI ya wagonjwa maalum na wakimataifa (Premier and International Patients’s services)
6. Aidha, katika kipindi hicho taasisi imetoa msamaha wa matibabu kwa wagonjwa 813.
7. Pamoja na mambo mengine Taasisi ya MOI imeendelea na utekelezaji miradi ya kimkakati ya Jengo jipya la wagonjwa wa nje (New OPD) na mradi wa X-Tumaini ambapo itaiwezesha MOI kuhudumia zaidi ya 1,500 kwa siku kutoka 500-700 wanaohudumiwa hivi sasa.
Hivyo, hali ya utoaji wa huduma katika Taasisi ya MOI ni nzuri, ikizingatia ubora, kasi ya huduma bora kwa wateja.
Kwa taarifa au maelezo ya kına kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi ya MOI wasiliana nasi kupitia:
+255/ 0733803104 huduma kwa wateja
+255/ 0733803104 WhatsApp.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!