Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Eng. Himba Atuhumu Kamati ya Uchaguzi TFF kwa Upendeleo na Ukosefu wa Uwazi

  • 8
Scroll Down To Discover

Mhandisi Mustapha Himba

Mdau wa mpira wa miguu nchini, Mhandisi Mustapha Himba, ameibuka na tuhuma nzito dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), akidai kuwepo kwa ukosefu wa uwazi katika mchakato wa kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho hilo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Juni 19, 2029 baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 16, 2025 jijini Tanga, Eng. Himba alieleza kusikitishwa kwake na kile alichokiita “mchakato usio wa haki na wenye viashiria vya upendeleo”.

“Tangu nimechukua fomu, nimekutana na changamoto nyingi. Nimehangaika mwenyewe kwa jitihada zangu zote kutafuta wadhamini (endorsement), nimepiga simu kila sehemu, lakini kila ninayempigia anasema ameshatoa. Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo, endorsement 47 tayari zimeshachukuliwa,” alisema kwa uchungu.

Eng. Himba alienda mbali zaidi kwa kumtuhumu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kwa “kuudanganya umma” kwa kuruhusu wagombea kuchukua fomu ilhali nafasi za wadhamini zikiwa tayari zimekwisha.

“Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi anakuja mbele ya vyombo vya habari na kuwaambia watu wachukue fomu, lakini wanajua endorsement zote zimeshachukuliwa. Hii ina maana tunaochukua fomu tunatoa sadaka!” alilalamika.

Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa TFF, kila mgombea anatakiwa kupata idadi fulani ya wadhamini kutoka vyama vya mikoa au vilabu ili kukidhi vigezo vya kugombea. Eng. Himba amesema hali ya sasa inaashiria kuwa tayari kuna mpango wa kuwabana baadhi ya wagombea wasifikie hatua ya kuwania nafasi hiyo kwa haki.

“Mimi sitakubali kutoa laki tano yangu halafu iwe kama nimechangia mapato ya TFF. Sifanyi hisani, nataka haki.” alisisitiza.

“Hatutanii na wala mimi sijawahi kutania, mimi ninachokihitaji Uchaguzi uwe huru na uwe wa haki, mimi sitaenda mahakamani kwasababu najua hairuhusiwi kwenda mahakamani hivyo nitafuata taratibu sahihi ili kupata haki yangu.”- Eng. Mustapha Himba.

Kauli ya Eng. Himba imeibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka nchini, huku wengine wakitaka TFF kujibu madai haya kwa uwazi ili kulinda heshima ya mchakato wa uchaguzi wa shirikisho hilo.

SIMULIZI ya MAMA YAIBUA HISIA KALI KAMPENI ya SAMIA LEGAL AID – “NDOA YANGU IMEVURUGWA -MSIJIFUNGIE”



Prev Post Ziara ya Rais Samia Yamalizika kwa Mafanikio Makubwa Simiyu – (Picha +Video)
Next Post Rais wa Israel Atoa Tamko Zito Baada Ya Shambulio La Iran Kulenga Hospitali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook