

Jeshi la Iran (Artesh) limeripoti kuangusha ndege ya tatu ya kivita aina ya F-35 inayomilikiwa na utawala wa Israel, kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa anga iliyotengenezwa ndani ya Iran.
Kwa mujibu wa tamko rasmi la Jeshi, rubani wa ndege hiyo ya kisasa kabisa iliyoundwa Marekani alikamatwa akiwa hai baada ya kujirusha kwa parachuti katika maeneo ya magharibi mwa Iran.
Kwa tukio hili, Iran sasa imefanikiwa kuangusha jumla ya ndege tatu za kivita za F-35 tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi Iran siku ya Ijumaa. Kati ya ndege mbili zilizoangushwa awali, imedokezwa kuwa rubani mmoja aliuawa papo hapo, huku mwingine akikamatwa na vikosi vya Iran.
Vita kati ya Iran na Israel vimechacha kufuatia mauaji ya takribani raia 100, maafisa wa kijeshi, na wanasayansi wa nyuklia wa Kiirani, waliouawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Israeli dhidi ya makazi ya raia mjini Tehran. Wakati wa kuanzisha vita hiyo, Israel ililenga maeneo nyeti ya nyuklia pamoja na kambi kadhaa za kijeshi kote nchini Iran.

Iran, kwa upande wake, imetoa jibu kali kwa mawimbi matano ya makombora ya masafa marefu kuelekea Israel, na kusababisha uharibifu mkubwa katika zaidi ya vituo 150 vya kijeshi na ujasusi ndani ya ardhi hiyo inayokaliwa kwa mabavu. Kwa sasa, Iran inaendeleza mashambulizi kwa kutumia droni za kujitoa mhanga (Kamikaze), huku duru za kijeshi zikidokeza kuwa mashambulizi makali zaidi kwa makombora yanatarajiwa kufuata ndani ya saa chache zijazo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!