

Edgar Lungu, ambaye aliongoza Zambia kutoka mwaka 2015 hadi 2021, alifariki Alhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 68, lakini kumezuka mvutano kati ya familia yake, serikali na chama cha siasa cha Lungu, Patriotic Front (PF), kuhusu wapi azikwe.
Mvutano huo umewaacha waombolezaji wakiwa wamechanganyikiwa kuhusu mazishi na jinsi gani hasa rais huyo wa zamani anapaswa kupewa heshima yake ya mwisho.
Serikali ilitangaza kuwa kutakuwa na mazishi ya kitaifa na kutangaza kwamba mahali rasmi pa maombolezo itakuwa sehemu ya kulala wageni inayomiliki katika mji mkuu, Lusaka, lakini chama cha PF kilitupilia mbali mpango huu, na badala yake, kikaelekeza waombolezaji waende kwenye makao yake makuu.
Kuhusu familia ya Lungu, wamesema hawapingi mazishi ya serikali, lakini wamesisitiza kuchagua ni nani atakayesimamia mazishi hayo, wakili wa familia Makebi Zulu ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC.
Katika msiba huo kuna utata wa kitabu cha maombolezo kwani vipo viwili, kitabu rasmi cha maombolezo ambacho waombolezaji wanaweza kusaini ili kumuenzi Lungu.
Serikali imetenga kitabu rasmi – katika eneo la kiserikali walilolitenga lakini chama cha PF kimewataka watu kusaini kitabu chao walichokiweka makao makuu ya chama.
Serikali ilitaka kurudisha mwili wake kutoka Afrika Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita. Lungu alifia huko baada ya kupata matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa.
Hata hivyo, chama cha PF na familia ya Lungu waliingilia kati, wakitaka kupewe fursa ya kufanya maandalizi wanayotaka kwa kiongozi huyo wa zamani.
“Serikali ilikuwa ikisema, ‘Tunampa heshima kamili ya kijeshi, kwa hivyo tutachukua mwili kuanzia hapa’ – kana kwamba wanasema ‘hamna uamuzi juu ya kile kinachotokea,'” alisema wakili wa familia, Makebi Zulu.
Mipango ya kurejesha mwili wa Lungu bado haijulikani utaletwa lini japokuwa familia sasa inashirikiana na serikali kuhusu suala hilo. Kuhusu familia ya Lungu, wamesema hawapingi mazishi ya serikali, lakini wamesisitiza kuchagua ni nani atakayesimamia mazishi hayo, kwa mujibu wa wakili wa familia, Makebi Zulu.
Kifo chake kimewashtua Wazambia – na kuna hali ya huzuni ya kweli huku vituo vyote vya redio vikipiga muziki wa injili kwa kiongozi huyo ambaye alikuwa amebakia kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Zambia licha ya kuzuiwa kugombea uchaguzi wa mwaka jana.
Zambia ni rasmi nchi ya Kikristo – na watu wengi huchukulia dini na vipindi vyao vya maombolezo kwa umuhimu mkubwa.
Serikali ilitangaza kipindi cha siku saba cha maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumamosi iliyopita, ingawa PF ilitangaza siku moja kabla na kipindi chote cha maombolezo hakutakuwa na aina zozote za burudani kama vile mechi kubwa za kandanda na matamasha kwani zimesimamishwa.
Kutoelewana kati ya serikali na familia kunaonekana kuwa mwendelezo wa uhusiano wa misukosuko kati ya Lungu na mrithi wake na Rais Hakainde Hichilema.
Wawili hao walikuwa ni wapinzani wa muda mrefu – mnamo 2017, Lungu alipokuwa rais, Hichilema aliwekwa kizuizini kwa zaidi ya siku 100 kwa tuhuma za uhaini baada ya msafara wa Hichilema kudaiwa kukataa kumpisha njia.
Ilibidi Jumuiya ya Madola kuingilia kati na Hichilema kuachiliwa huru. Miaka minne baadaye, na baada ya majaribio matano ya urais, Hichilema alimshinda Lungu.
Na Elvan Stambuli GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!