Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Viongozi na Wanachama CHADEMA Kilimanjaro Watimkia CCM

  • 31
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujivunia wanachama wapya kutoka katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wanachama hao wamepokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amepokea wanachama hao wapya akiwa katika mikutano ya hadhara aliyoifanya akiwa katika ziara yake ndani ya Wilaya mbili za Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Mjini na Rombo.

Akiwa Moshi Mjini Makalla amepokea wanachama 23 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa kutoka katika Kata ya Bondeni wilayani Hai, Dastan Kimaro.

Akifafanua sababu za kurudi CCM Kimaro amesema akiwa kama kiongozi amekuwa hapati ushirikiano kwani hakuwa na viongozi wa kutoka katika chama chake pia hakuwa na ilani aliyokuwa akiitekeleza kwa sababu sera anazotakiwa kuzitekeleza ni za Ilani ya CCM.

“Sikuona Ilani yoyite ya Chadema amabayo ilikuwa katika utekelezaji nikagundua kuwa sera zote ninazotakiwa kuzitekeleza ni cha chama za mapinduzi ndipo nilipoamua kurudi katika chama cha Mapinduzi,” amesema Kimaro.

Pia Makalla akiwa akizungumza na wananchi katika eneo la Tarakea wilayani Rombo amepokea makada wengine wa Chadema 15 wakidai kuikataa vikali kauli ya ‘No reform no election’ na kuamua kutimkia CCM.



Prev Post Viongozi na Wanachama CHADEMA Kilimanjaro Watimkia CCM
Next Post Vodacom Tanzania Yazindua Kampeni ya Kuadhimisha Miaka 25, Yabeba Ujumbe “Tupo Nawe, Tena na Tena”
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook