

Dar es Salaam, 8 Juni 2025: Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini 2020 na kuambulia nafasi ya pili ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara mpaka sasa, Faustine Matiku amejitokeza kutia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kivule, Dar.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo, Matiku amesema ameamua kutumia fursa hiyo ya kugombea jimbo hilo jipya ambalo yeye kama mkazi wa eneo hilo na kuahidi kuanza kwa kuboresha maendeleo kwenye jimbo hilo jipya.
Baadhi ya mambo aliyosema ataanza nayo ni pamoja na kuboresha ufugaji wa kuku kisasa na kuanzisha soko la kisasa kwenye jimbo hilo ambalo wakazi wake wengi ni wajasiriamali wa biashara ya ufugaji na uuzaji wa kuku na mayai.
katika uboreshaji wa biashara hilo Faustine amesema atahakikisha wajasiriamali hao wanapata chakula cha mifugo yao pamoja na madawa kwa bei rafiki tofauti na ilivyo sasa wanavyouziwa kwa bei mbaya na kuwanyima faida kubwa.
Pamoja na hayo ameahidi kuboresha nyanja zingine za kimaendeleo kwenye jimbo hilo na kulifanya kuwa na maendeleo makubwa kuliko ilivyo sasa. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!