Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Akatwa Koromeo Kimakosa Akifanyiwa Operesheni Ya Goita Hospitalini – Video

  • 33
Scroll Down To Discover

Hakika ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Ibrahim Farijallah, mkazi wa Survey, Chuo Kikuu, jijini Dar es Salaam, anakabiliwa na changamoto kubwa baada ya kukatwa baadhi ya mishipa ya hewa kooni wakati wa upasuaji wa goita ya ndani (thyroid gland). Tukio hilo lilimsababishia hali mbaya kiafya, ambapo sasa analazimika kutumia mashine maalumu aliyowekewa shingoni kwa ajili ya kupumua.

Hadi sasa, Ibrahim anahitaji kiasi cha shilingi milioni 34 kwa ajili ya matibabu nchini India ili kurejesha hali yake ya kawaida. Kwa bahati mbaya, hospitali iliyohusika na makosa hayo ilimlipa fidia ya shilingi milioni nne tu, kiasi ambacho hakitoshelezi hata robo ya gharama za matibabu yanayohitajika. Hali hii imemfanya kusimamisha shughuli zake zote za kiuchumi, huku akiwa baba wa familia inayomtegemea.

Kama umeguswa na habari ya Ibrahim, unaweza kumsaidia kwa kuchangia kupitia namba zifuatazo: 0713777067/0740944777

(Jina: Ibrahimu Farijallah)



Prev Post Mama Mzazi wa Carina, Fatma Maruzuku, Afariki Dunia Siku 40 Baada ya Kifo cha Mwanaye
Next Post Mchengerwa: Hakuna Fursa Kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano Kubadili Shule Walizopangiwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook