Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto: Watanzania kataeni kugawanywa kwa Udini na Ukabila

  • 10
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakuna na wala hatokei mtu yeyote atakayethubutu kuwagawa Watanzania aidha kwa ushawishi wa Dini, Ukabila au Ukanda.

Chama hicho pia kimewahakikishia Watanzania , Amani na Umoja wa Kitaifa uliojengeka ,hakutokani na dhamana ya mtu mmoja , dini fulani, kabila au kanda yoyote.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo huku akiahidi hatokei yeyote mwenye misuli ya kulipasua Taifa.

Mbeto alisema kutokana na Waasisi wa taifa kutoa jasho jingi ,kupoteza ,maishha , nguvu na jasho lao jingi ,hakuna Mtanzania aliye tayari kuona Taifa likigawanywa na vibaraka wachache.

Alisema Tanzania imejengwa kwa nguvu ya Dini zote, Makabila na Wananchi kuanzia Vijiji ,Kata, Wilaya na Mikoa yote, hivyo dhamana ya kulihami na kulilinda Taifa hili , itabaki mikononi mwao wenyewe.

‘Chama chetu kinawahakikshia hatatokea mtu yeyote au kikundi litakalowagawa Watanzania aidha kwa ushabiki wa Dini, Ukabila au Ukanda. Taifa letu litaendelea kubaki imara na kuwa moja milele’ Alisema Mbeto

Aidha, Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema na kutaja hatua ya kuchomoza kedi na vitimbi vya baadhi ya watu wanaodhani wana ubavu wa kukoleza kuni za uchochezi huku akisema watu hao wataaibika.

“Tumeshuhudia yaliotokea kwa majirani zetu pia Taifa la Afrika ya Kati. Tunajua hatari na hasara ya mivutano ya Udini na Ukabila. Hakuna atakayelala kitandani kwake akawaacha manyang’au wakilipasua Taifa “Alisisitiza Mbeto

Aidha alisema wakati huu nchi ikielekea katika Uchaguzi mkuu, watachomoza watu mapepe watakaofanya majaribu wakidhani dola itakuwa imelala , hivyo akawataka wajue kila dola duniani ina pua zake, macho, midomo na masiko .

“Tulumbane na kucharuana kwenye majukwaa ya Kisiasa bila kuamsha hisia za dini, ukabila au ukanda. Atakaepita kwenye barabara hizo atakutana na baladia zenye miba na misumari ” Alieleza

Akizungumza kwa undani, Mbeto alisema ikiwa kuna Wanasiasa ambao waliopeteza amana na mtaji ya kisiasa katika jamii, waache kutumia Lugha za ukabila na udini kwani hayupo atakayewavumilia.

Mbeto alisema Watanzania ni werevu hivyo hawako tayari kutumika katika ushabiki wa hovyo huku wakiliacha Taifa lao likipoteza Amani ,Umoja na Mshikamano.



Prev Post BAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPA…AZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA..
Next Post Mama Mzazi wa Carina, Fatma Maruzuku, Afariki Dunia Siku 40 Baada ya Kifo cha Mwanaye
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook