Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Iran Yatoa Mwito wa Kusitishwa Mapigano Gaza

  • 34
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ametoa mwito wa kusitishwa haraka mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza na kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wananchi wa Ukanda huo.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo akiwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo kwenye awamu ya kwanza ya safari yake ya kutembelea nchi mbili za ukanda huo na amepongeza juhudi za Misri na Qatar za kupigania kukomeshwa mashambulizi ya Israel huko Ghaza. Amesema hayo mbele ya waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty jana Jumatatu.

Amesema: “Iran inaunga mkono [makubaliano] yoyote ya kusitisha mapigano ambayo watu wa Ghaza watayakubali.”

“Tunatumai kwamba usitishaji vita endelevu utafikiwa [huko Ghaza] haraka iwezekanavyo, zoezi la kubadilishana mateka litafanyika na misaada ya kibinadamu itaingia Ghaza. Tunatamani marafiki zetu nchini Misri wapate mafanikio katika juhudi zao kwenye suala hili,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akiwa mjini Cairo.

Wiki iliyopita, Televisheni ya Al Jazeera ilinukuu duru ambazo hazikutajwa jina zikisema kwamba Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na mjumbe maalumu wa Marekani, Steve Witkoff wamefikia mwafaka juu ya kanuni ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa namna ya kudumu katika Ukanda wa Ghaza, hatua ambayo huenda ikafungua njia ya kumalizika vita vya miezi 19 kwenye Ukanda huo uliozingirwa kila upande.

Vilevile Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Cairo hivi sasa uko kwenye mkondo mzuri. Aidha amesema, Iran inaandaa majibu ya mapendekezo ya Marekani kuhusu mazungumzo ya nyuklia.



Prev Post Mbeto: Askofu Gwajima Alitaka Unaibu Waziri Kwa Rais Samia Akanyimwa – Video
Next Post Polisi Watekeleza Agizo la Kusitisha Shughuli za Kanisa la Askofu Gwajima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook