Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbosso Anakuja Na Jambo Gani ?

  • 34
Scroll Down To Discover

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi almaarufu kama Mbosso, amewashangaza mashabiki wake baada ya kuvunja ukimya wake wa muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram. Hii ni baada ya kufuta post zake zote katika ukurasa wake rasmi wa Instagram, kitendo kilichoacha mashabiki na wadau wa muziki wakijiuliza maswali mengi kuhusu kinachoendelea kwenye maisha ya msanii huyo.

Leo hii, Mbosso amerudi tena mtandaoni kwa kishindo kwa kushiriki picha moja tu yenye mandhari ya rangi ya kijani kibichi, rangi ambayo wengi wanaamini ina ujumbe mzito au wa kisanii. Picha hiyo haikuambatana na maelezo yoyote, jambo lililozidisha uvumi na kuibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake, wakitaka kufahamu nini hasa kinachojiri nyuma ya pazia.

The post Mbosso Anakuja Na Jambo Gani ? appeared first on Wasafi Media.



Prev Post Rihanna Afiwa Na Baba Yake Mzazi ‘Ronald Fenty’.
Next Post Balozi Nchimbi Awasili Songea Mazishi Ya Mzee Songambele
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook