
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimewaalika wananchi wote, mashirika ya kiraia, Jumuiya za Kimataifa na Kitaifa kuhudhuria na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.
Kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar Es Salaam kesho Jumatatu Juni 02, 2025, kuanzia saa tatu asubuhi.
Wito wa kuhudhuria kesi hiyo umetolewa na John Wegese Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, akisema kwamba huu ni wakati wa kuonesha mshikamano na kusimama kidete kwaajili ya kulinda misingi ya haki, uhuru na utawala wa sheria nchini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!