

Mwili wake ulikuwa dhaifu, na mara nyingi alilala kitandani bila kuweza hata kufanya kazi ndogo. Wakati wenzake walikuwa wakihangaika mashambani au sokoni, yeye alibaki nyumbani akilia kwa maumivu.
Wazazi, ndugu na hata marafiki walijaribu kila mbinu kumsaidia. Alitembea hospitali nyingi, akaandikiwa dawa zisizo na mwisho.
Wakati mwingine alijisikia nafuu kwa muda, lakini baada ya siku chache hali yake ilirudi pale pale. Madaktari walikuwa wameshindwa kueleza hasa ni ugonjwa gani ulimuandama.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!