Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa Zamani wa Marekani Joe Biden Agundulika na Saratani ya Tezi Dume

  • 41
Scroll Down To Discover

Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden

Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, amethibitishwa na ofisi yake kuwa amegundulika kuwa na aina kali ya saratani ya tezi dume ambayo imeenea hadi kwenye mifupa. Ugonjwa huo umetambuliwa kuwa na alama ya Gleason 9, ikionyesha kuwa ni aina ya saratani inayokua kwa haraka na kwa ukali mkubwa. Hata hivyo, madaktari wake wamesema kuwa saratani hiyo ni nyeti kwa homoni, jambo linalowezesha usimamizi wa matibabu kwa ufanisi.

Biden, mwenye umri wa miaka 82, alipata uchunguzi baada ya kuonyesha dalili za matatizo ya mkojo, ambapo kipimo kilibaini uvimbe kwenye tezi dume. Baada ya vipimo zaidi, aligundulika kuwa na saratani hiyo siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa sasa, yeye na familia yake wanashauriana na madaktari kuhusu chaguzi za matibabu.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), saratani ya tezi dume ni ya pili kwa kuathiri wanaume baada ya saratani ya ngozi. Umri mkubwa ni miongoni mwa sababu kuu za hatari ya kupata ugonjwa huu.

Kwa sasa, Biden na familia yake wanaendelea kushauriana na madaktari kuhusu njia bora za matibabu.

Stori na Elvan Stambuli, GPL

LEMA – BONI YAI na JENERALI ULIMWENGU WAKIINGIA MAHAKAMANI KESI ya LISSU KISUTU….



Prev Post SERIKALI YA TANZANIA YAIJIBU BUNGE LA ULAYA: YASIMAMA KIDETE KULINDA UHURU WA TAIFA NA MAFANIKIO YA DEMOKRASIA
Next Post Shigongo Awachana Vijana Wa Buchosa “Hatuwezi Kuwa Na Taifa Lenye Ulevi Na Kubeti…” – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook