
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kuwa Jeshi la Polisi linafuatilia kwa makini kauli zinazotolewa na baadhi ya watu zinazohusiana na maandamano au kampeni zinazohusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akizungumza kwenye Mdahalo wa Wadau wa Amani, uliofanyika jana Agosti 20, 2025, Kamanda Muliro alisema:
“Jeshi la Polisi tunazifuatilia kwa karibu kauli ya Oktoba Tunatiki na No Reforms No Election. Ukiwa unasema No Reforms No Election, basi hiyo ni kwa Sheria gani? Oktoba Tunatiki maana yake ni ‘sawa’ kwa tafsiri ya alama…”
Aliongeza kuwa ufuatiliaji huu unalenga kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazohusiana na uchaguzi zinafanyika kwa madhubuti, kwa amani, na kwa mujibu wa sheria.
Kamanda Muliro pia aliwataka wadau wote wa uchaguzi, wakiwemo wanaharakati na wanasiasa, kuhakikisha maneno na vitendo vyote vinavyohusiana na kampeni au maandamano vinatimizwa kwa njia ya amani.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!