Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kihongosi Ateuliwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa

  • 6
Scroll Down To Discover

Kenan Kihongosi, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, imemteua Kenan Kihongosi, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho kuanzia Agosti 23, 2025.

Uteuzi huo umetangazwa baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika jijini Dodoma, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, uteuzi wa Kihongosi ni sehemu ya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya CCM yenye lengo la kuimarisha shughuli za kisera, kueneza sera za chama na kuboresha mawasiliano ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wake umezingatia uwezo wa kiuongozi, uzoefu katika masuala ya kisiasa na uaminifu aliouonesha katika nafasi mbalimbali ndani ya chama.

Kihongosi anatajwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyekaa kwa muda mfupi zaidi, kwani aliteuliwa Juni 23, 2025, na baada ya miezi miwili tu, Agosti 23, 2025, ameteuliwa kushika nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa.



Prev Post Rais Samia Amteua Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Next Post Mashirika ya Umma Yatambuliwa Kwa Ufanisi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook