
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua CPA. Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, ikibainisha kuwa Makalla anachukua nafasi ya Bw. Kenan Laban Kihongosi.
Kihongosi, ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amehamishwa CCM ambapo ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi.
Kabla ya uteuzi huu, Makalla alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, nafasi aliyoitumikia hadi mabadiliko yaliyotangazwa na Halmashauri Kuu ya CCM usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Shaaban Kissu, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, uapisho wa Mkuu wa Mkoa mteule utafanyika tarehe 26 Agosti 2025, saa 5:00 asubuhi, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!