Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wakurugenzi Wahimizwa Kutenga Fedha Kwaajili Ya Ujenzi Wa Miradi

  • 32
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Zainab Katimba

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Zainab Katimba amesema serikali itaendela kusimamia Halmashauri zote nchini ili ziweze kutimiza majukumu ya msingi ya kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu.

Mhe. Katimba amesema hayo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Mhe. Mwita Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini aliyeitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutoa muongozo kwa Halmashauri kwa mwaka wa fedha ujao ili kila Halmashauri iweke mpango wa kumaliza tatizo la meza, viti na madawati.

Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amesema “Nitumia nafasi hii kuendelea kutoa msisitizo kwa wakurugenzi wetu wa halmashauri zote 184 waweze kutimiza wajibu wao wa msingi wa kutenga fedha kutoka kwenye mapato ya ndani na kuweza kuziweka kwenye mipango na bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo” Amesema

Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amesema kwa mwaka wa fedha 2025/26 serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 613 pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo upatikanaji wa madawati.



Prev Post BoT yasisitiza marufuku matumizi ya fedha za kigeni kwenye miamala ya ndani Tanzania
Next Post Benki ya Azania Yakabidhi Madawati 200 Kwa Shule za Msingi na Sekondari Musoma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook